logo

MATAYARISHO YA KONGAMANO LA UGATUZI YASHIKA KASI

Naibu Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu Mhandisi John Barorot amethibitisha kuwa matayarisho ya Kongamano yameshika kasi katika kila sehemu kuanzia Shule ya Hill school,Sports Club,Uwanja wa Michezo wa Kipchoge na Bustani la mji wa Eldoret na kutoa hakikisho kuwa Idara zote husika zinafanya kazi kwa uwiano Ili kufanikisha kongamano.

Akiongoza kikao cha wawakilishi wa baraza la magavana na maafisa wa Kaunti hii,Naibu Gavana ameonyesha kuridhika kwake na hatua zilizofikiwa katika matayarisho hadi sasa.

” Kuna marekebisho na uboreshwaji wa barabara na njia ndogo mjini,ujenzi wa milingoti zenye taa kule sports club na ujenzi wa lango kuu pamoja na sehemu za maji na umeme wenye nguvu” alisema Barorot.

Naibu Gavana alieleza kuwa njia za Racecourse zarekebishwa na kusambaza mwangaza wa kutosha na vilevile kuhakikisha njia za kutembelea kwa miguu zimeimarishwa na kwamba sehemu hiyo imetengwa kwa minajili ya biashara.

Kamishna wa Uasin Gishu Dkt Eddyson Nyale alikiri kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa usalama wa kutosha umeimarishwa sasa na wakati wa kongamano.

“Tunashirikiana na maafisa wa Kaunti kuhakikisha kuwa wajumbe,wageni na wakaazi wote wa Uasin Gishu watakaoshiriki kongamano watanufaika na usalama wa kutosha.”

Wawakilishi wa baraza la magavana na maafisa wa Kaunti walikubaliana sehemu zinazohitaji kufanyiwa marekebisho ili kufanikisha kongamano